Unachotakiwa kufanya ni kufanya Setting kabla jambo lolote baya halijakutokea.
Fanya kama ifuatavyo:
Kwanza nenda kwenye setting menu na kubofya kwenye Security.

Kisha tafuta “Android Device Manager" au inaweza kuwa “Device Administrators" kwenye android version ya zamani.

Sasa bofya kwenye Device Administrators na uweke tick kwenye “Android Device Manager" option.

. kwa ku-check option hii utakuwa na uwezo wa kujua simu yako ilipo remotely kwa kupitia GPS, unaweza kuifanya simu yako iite kwa dakika tano na pia unaweza kuifunga (lock) screen ya simu yako au kufuta (erase) data zako zote.

Kama unapata shida tembelea Google.com/android/devicemanager.

Na unaweza kujua mahali halisi ilipo simu yako, kuifanya iite au kufuta kila kitu kilichomo kwenye simu.

Kwa njia hii unaweza kuipata simu yako kwa urahisi. Tafadhali usisahau ku-share hii post kwa wenzako na endelea kutembelea mtandao huu kila siku ili upate mbinu zingine nyingi kuhusu mambo mbalimbali muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.

Interesting Article. Hoping that you will continue posting an article having a useful information. IT Services Berlin
ReplyDelete