JIFUNZE NAMNA YA KUIFUNGIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KWA MUDA BILA KUITUMIA? CHEKI HAPA JINSI YA KUFANYA





Kama unahisi umetosheka na hutaki kuwa na akaunti yako ya Facebook tena? Kama jibu NDIO basi una namna mbili za kufanya. Unaweza kuifungia akaunti yako ambapo wasifu wako utatoweka mtandaoni lakini taarifa zote kwenye akaunti yako zitahifadhiwa kwenye mitambo ya Facebook endapo kama utataka kurudi na pia unaweza kuifuta akaunti yako moja kwa moja ambapo inamaanisha kuwa taarifa zako zitaondolewa na hutaweza kuitumia tena akaunti hiyo.

Hivi ndivyo unaweza kuifungia akaunti yako bila kujali kama utataka kurudi au hutataka kurudi:

Kuifungia (Deactivation) akaunti yako kwa muda inamaanisha kuwa una nafasi ya kurudi Facebook muda wowote unaotaka.
Bonyeza mshale unaoangalia chini ambao upo upande wa juu upande wa kulia wa ukurasa wako wa Facebook
Chagua “Settings”
Bonyeza “Security kwenye upande wa kushoto
Chagua “Deactivate your account” kisha fuata hatua zilizoorodheshwa

Ukiifungia akaunti yako inamaanisha kuwa wasifu wako hautaonekana kwa watu wengine na watu hawataweza kukutafuta lakini baadhi ya taarifa kama vile jumbe zilizotumwa kwa marafiki zinaweza kuonekana kwa wengine.

Kama utataka kurejesha akaunti yako unaweza kuifungulia muda wowote kwa kuweka email na nywila yako. Ukurasa wako utarudishwa ukiwa na taarifa zako zote.
Share on Google Plus

About IT MAN SOLUTION

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment