Je ? Wajua jinsi ya kutumia account yako ya Gmail kupata simu yako ya Android smartphone iliyoibiwa

Suala la kuibiwa simu au kupoteza ni la kawaida na huwatokea wengi ndio sababu hapa leo nataka kukupa moja kati ya njia unayoweza kutumia kufuatilia simu yako iliyopotea au kuibiwa. Kama una simu ya android smartphone, Google ina kitu kipya kwa ajili yako ambacho kinakusaidia kuipata simu yako. Au kama sio kuipata basi angalau unaweza kufuta data zako zote zilizomo kwenye simu hiyo iliyopotea au kuibiwa kwa hivo alieiba simu yako hatoweza kutumia taarifa zako za kwenye simu kwa mambo mabaya.


Unachotakiwa kufanya ni kufanya Setting kabla jambo lolote baya halijakutokea.


Fanya kama ifuatavyo:
Kwanza nenda kwenye setting menu na kubofya kwenye Security.

Kisha tafuta “Android Device Manager" au inaweza kuwa “Device Administrators" kwenye android version ya zamani.

Sasa bofya kwenye Device Administrators na uweke tick kwenye “Android Device Manager" option.

. kwa ku-check option hii utakuwa na uwezo wa kujua simu yako ilipo remotely kwa kupitia GPS, unaweza kuifanya simu yako iite kwa dakika tano na pia unaweza kuifunga (lock) screen ya simu yako au kufuta (erase) data zako zote.

Kama unapata shida tembelea Google.com/android/devicemanager.

Na unaweza kujua mahali halisi ilipo simu yako, kuifanya iite au kufuta kila kitu kilichomo kwenye simu.

Kwa njia hii unaweza kuipata simu yako kwa urahisi. Tafadhali usisahau ku-share hii post kwa wenzako na endelea kutembelea mtandao huu kila siku ili upate mbinu zingine nyingi kuhusu mambo mbalimbali muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Share on Google Plus

About IT MAN SOLUTION

    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Interesting Article. Hoping that you will continue posting an article having a useful information. IT Services Berlin

    ReplyDelete